Nitasimama Mpaka Unipende (Swahili Poem)

Listen to the poem Nitasimama Mpaka Unipende

Nitasimama,
kima cha urefu wa mbingu,
na nyota zake hewani,
mpaka nisimame wima.

Nitasimama,
kutoka kwenye uoga,
wa niliyemchagua,
lakini akaninyamazisha uhuru wangu.

Nitasimama,
kutoka kivuli,
cha aliyenioa,
lakini akanitia aibu hadharani.

Nitasimama,
kutoka kwenye mapenzi,
ya niliyempenda,
lakini akanilaani kwa mauaji ya halaiki.

Nitasimama,
kutoka kwenye ngao,
za niliyemkimbilia,
lakini akanikabidhi kwenye ulemavu.

Nitasimama,
kutoka mikono michafu,
ya yule niliyemuamini,
lakini akanibaka bila huruma.

Nitasimama,
kima cha urefu wa utukufu,
na sifa ya utu wangu,
mpaka unipende.

*Shairi hili limehamasishwa na ujumbe wa siku ya Valentine mwaka huu ambayo ni siku wanawake billioni moja duniani tunahamasishwa kusimama, kudansi na kutokomeza ukiukaji dhidi ya wanawake.

6 Comments
 • Halima Mhando
  Reply

  Nicely writen. lakini kwa kusoma umesema (lakini akaninyamazisha) ila umeandika.. Sasa sijui kama ni typing mistake au ulimean kitu kingine. Congrat, it’s lovely.

  Nitasimama,
  kutoka kwenye uoga,
  wa niliyemchagua,
  lakini akaninyamiza uhuru wangu.

  12/02/2013 at 12:42
 • Agnes Leandri
  Reply

  Love the poem! Happy Valentines!

  13/02/2013 at 10:51
 • Asante kwa shairi zuri sana, ila katika Kiswahili mashairi ya masivina hayana mvuto sana japo yanavutia. Hebu jaribu kutunga ya kimapokeo uone jinsi yanavyovutia kwa utamu wa lugha na mnato wa sauti. All in all hongera sana.

  09/06/2014 at 21:17

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.