Chini Ya Mwembe

Binadamu akiwa na fikra hutafuta mahali akae kimya na kutafakari kwa makini. Moja ya sehemu mwanana ni chini ya mwembe. Mti wa mwembe hauchagui nani aketi chini yake. Utampa kila mtu faraja ya tunda, kivuli au yote.

Tafakari chini ya mwembe yaweza leta hisia mbalimbali. Ukisikia ndege wanaimba labda nawe pia utaimba. Majani ya mwembe yakipuliza na upepo mwanana, labda nawe utapata utunzi wa faraja. Chini ya mwembe, kalamu ya moyo wako yaweza andika fikra zozote.

Chini ya Mwembe ni kusanyiko la mashairi tofauti yanayogusa maisha ya mwanadamu. Mashairi yaliyopo yanatambua hisia mbalimbali kama mapenzi, furaha, amani, wasiwasi, uchungu, hasira, n.k. Maisha bila hisia ni kifo. Kitabu hiki kina nia ya kukuhamasisha nawe utafute mti wako wa mwembe utakaokusaidia kutafakari hisia za maisha.

Kitabu kinapatikana Mwenge Catholic University (MWECAU), Moshi, simu namba 0755 978 786

Karibu chini ya mwembe!

CATEGORY
Poetry