Shairi: Je, Wewe Ni Mbaguzi?

Picha na Nick Bolton kutoka Unsplash

Unapofikiria yeye ni:
mshamba
wa kuja
wa mjini
wa kijiweni
mvutaji
tajiri
maskini.

Unaposema yeye hana:
mtindi
wowo
mwili
unywele.

Unaposema yeye ana:
ubapa
mianzi
tege
njiti
kipilipili.

Unapomuita yeye ni:
bundi
jalala
cheupe
cheusi
shombe
mhindi koko
mzungu pori.

Je, wewe ni mbaguzi?

No Comments

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.